4 Julai 2026 - 13:31
Sala ya maiti ya Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei na familia yake kufanyika Jumapili asubuhi mjini Tehran

Kamati ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza kuwa sala ya maiti ya Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (r.a.) pamoja na baadhi ya wanafamilia wake na mashahidi wengine itafanyika Jumapili saa 12:00 asubuhi kwa saa za Iran katika Msala wa Tehran.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kamati ya Habari Rasmi ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza ratiba ya ibada ya sala ya maiti kwa ajili ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (r.a.), pamoja na baadhi ya wanafamilia wake na Mashahidi wengine.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ibada ya sala ya maiti itafanyika kesho, Jumapili, saa 12:00 asubuhi kwa saa za Iran katika Msala wa Tehran, na kuhudhuriwa na viongozi wa kisiasa, wanazuoni wa dini, pamoja na maelfu ya wananchi na wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s.).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa sala hiyo itaswaliwa kwa ajili ya miili ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ali Khamenei, pamoja na Dkt. Misbah al-Huda Baqeri Kani, Bi. Bushra Khamenei, Bi. Zahra Haddad Adel, na Bi. Zahra Mohammadi Golpayegani, ambao wote wametajwa miongoni mwa mashahidi wa tukio hilo.

Sherehe za kuaga na mazishi ya Kiongozi Shahidi zinatarajiwa kuwa miongoni mwa matukio makubwa zaidi ya kihistoria katika ulimwengu wa Kiislamu, zikihudhuriwa na mamilioni ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sala ya maiti ya Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei na familia yake kufanyika Jumapili asubuhi mjini Tehran

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha